President Jakaya Mrisho Kikwete in conversation with the leader of the Ismailia Community His Highness Aga Khan at the Hyatt Regency London this afternoon (photo by Freddy Maro).
Kiongozi wa kidini wa Jumuiya ya Ismailia duniani Imam Aga Khan ameleezea nia yake ya kutaka kujenga chuo kikuu kipya hapa nchini.
Akizungumza na Makamu wa Rais Dk. Ali Mohamed Shein leo Ikulu Jijini Dar es salaam Imam Aga Khan amesema chuo hicho kitajengwa mkoani Arusha na kwamba kitakuwa cha aina yake katika Afrika kutokana na kuhusisha masomo ya taaluma muhimu pekee.
Alisema eneo limekwishapatikana na fedha kwa ajili ya kuanzia ujenzi wa chuo hicho tayari zimekwishatengwa.
Aidha Kiongozi huyo wa kidini alimweleza Makamu wa Rais kuwa mipango ipo mbioni ya kuanzisha shahada ya uzamili hadi shahada ya uzamivu (PHD) kwenye fani ya uuguzi katika chuo kikuu cha Aga Khan kilichoko Dar es salaam ili kuwawezesha wauguzi hapa nchini kupata elimu ya juu katika fani hiyo.
Aidha alisema kutokana na umuhimu wa afya kwa watanzania chuo hicho kimeanza kutoa stashahada ya uzamili kwenye masuala ya afya kwa umma.
Katika mazungumzo hayo Makamu wa Rais alitoa ombi la kutaka chuo kikuu cha Aga Khan kuangalia uwezekano wa kuweka programu ya magonjwa yasiyopewa kipaumbele (Neglected Tropical Diseases) ili kutokomeza maganjwa hayo jambo ambalo Imam huyo amesema ni zuri na kusisitiza kwamba njia inayofaa ni kuhusisha magonjwa hayo katika nyanja ya utafiti wa maradhi ya afya.
Dk. Shein alimshukuru Imam Aga Khan kwa misaada yake katika sekta mbali mbali ikiwemo ya elimu, afya, utalii kwa kuwa inasaidia jitihada za serikali katika kuwaletea maendeleo wananchi wake.
Alimpongeza kwa kutimiza miaka 50 ya uongozi wake katika Jumuiya ya Ismailia kiasi kwamba amepata mafanikio katika kuboresha ustawi wa jamii na kusaidia miradi katika nchi mbali mbali ikiwemo Tanzania.